Kongamano hilo limeandaliwa kwa ushiriki wa wajumbe na shakhsia kutoka mataifa mbalimbali kwa lengo la kujadili nafasi ya vyombo vya habari na riwaya ya simulizi katika kuutetea uwezo wa kadhia ya Palestina, sambamba na kutafuta ilhamu kutoka misingi ya mapinduzi ya Imam Hussein (AS) katika kukabiliana na upotoshaji wa ukweli na kueneza mwamko.
Karbala yaandaa Kongamano la 5 la Kimataifa la Nidaa al-Aqsa
Tukio hilo limeanza leo, Jumamosi, kwa kikao rasmi cha kwanza kilichojumuisha hotuba za waandaaji pamoja na wajumbe wanaoshiriki, kwa mujibu wa Al-Ahed News.
Baada ya hapo, kutafanyika kikao chenye anuani ya “Shuhuda za Moja kwa Moja; Riwaya ya Kweli Kutoka Katika Moyo wa Tukio”, ambapo ndugu wa mashahidi, wafungwa wa Kipalestina walioachiwa huru, majeruhi, pamoja na waandishi wa habari waliowasili kutoka Palestina watatoa ushuhuda wa nyaraka kuhusu matukio ya uwanjani katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Siku ya kwanza itahitimishwa kwa washiriki kufanya ziara katika haram ya Imam Ali (AS) mjini Najaf.
Katika siku ya pili, ratiba inajumuisha wajumbe kutembelea haram ya Imam Hussein (AS) na kupokelewa rasmi na uongozi wa Ataba Tukufu, kisha kusikiliza muhadhara wa kidini na kushiriki swala ya Adhuhuri kwa jamaa katika ua wa haram hiyo tukufu.
Mwisho, washiriki hao watashiriki katika uzinduzi wa Mawkib ya “Wito wa Al-Aqsa” kwenye njia ya mazuwaru kati ya Najaf na Karbala.
Abdul Malik Sukriyyah, katibu wa Kampeni ya Kimataifa ya Haki ya Kurejea Palestina, ameeleza kuwa kongamano hili linafanyika katika mazingira ya kipekee na licha ya vitisho vya Marekani dhidi ya eneo hili, kwa lengo la kusisitiza kuendelea kwa njia hii na kuangazia uhusiano kati ya qiyam ya Imam Hussein (AS) na yale yanayozikabili mataifa ya muqawama, hususan Ukanda wa Gaza.
3498405