IQNA

Iran yaanza rasmi kutuma Mazuwari Iraq kwa ajili ya Arbaeen

15:49 - July 26, 2026
Habari ID: 3482538
a
IQNA – Makao Makuu ya Kituo cha Arbaeen nchini Iran yametangaza kuanza rasmi kwa utumaji wa mazuwari kuelekea Iraq kwa ajili ya msafara wa Arbaeen wa mwaka huu.

Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi, makao hayo makuu yaliwapa mahujaji maelekezo na nasaha kadhaa kuhusu ushiriki katika hafla hii kubwa ya kiroho.

Taarifa hiyo imewataka mazuwari kuelekea kwenye mipaka ya kutokea nchini wakiwa na pasipoti halali ya kimataifa au pasipoti ya hija, yenye muda wa uhalali wa angalau miezi sita.

Aidha, imesema kuwa programu za utekelezaji na uendeshaji za mawakib, yaani vituo vya huduma vilivyopo kwenye njia za misafara ya mazuwar wa Arbaeen, zimeanza kufanya kazi tangu Julai 26, huku mazuwari wakihimizwa kushirikiana kikamilifu na wahudumu pamoja na maafisa waliopo njiani kwa ajili ya kuwahudumia mazuwaru.

Taarifa hiyo pia imewataka mahujaji kubeba dawa zao binafsi na dawa muhimu wanazohitaji, hasa wale wenye maradhi maalumu, kwa kiasi cha kutosha.

Ili kujiepusha na uchovu uliopitiliza, mahujaji wamehimizwa kutumia viatu vinavyofaa, kubeba mkoba wa mgongoni ulio bora na wa kawaida, na kusafiri wakiwa na mizigo mepesi.

Arbaeen ni munaasaba wa kidini unaoadhimishwa na Waislamu wa Kishia siku ya arobaini baada ya Siku ya Ashura, kwa kumbukumbu ya kuuawa shahidi kwa Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na Imam wa tatu wa Kishia.

Ni miongoni mwa zaiyara kubwa zaidi za kidini kila mwaka duniani, ambapo mamilioni ya Waislamu wa Kishia, pamoja na Masunni wengi na wafuasi wa dini nyingine, hutembea kwa miguu kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arbaeen itaangukia Agosti 4.

3498416

captcha