IQNA

Mtaalamu wa Qur’ani: Kiongozi Shahidi ni Kielelezo cha Maisha ya Qur’ani katika Zama hizi

11:35 - July 20, 2026
Habari ID: 3482513
A
IQNA – Mtaalamu na msomaji maarufu wa Qur’ani wa Iran amemuelezea Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, kama kielelezo cha maisha ya Qur’ani katika zama zetu za kisasa.

Akizungumza na IQNA, Abbas Salimi amesisitiza kuwa Kiongozi huyo Shahidi hawezi kuelezea kwa kutumia nyanja moja tu ya shughuli za Qur’ani.

“Utu wake, mawazo yake, mwenendo wake, usimamizi wake, na maisha yake yote yalijengwa kuzunguka mafundisho ya Wahyi. Alichukuliwa kuwa ni kielelezo cha maisha ya Qur’ani katika zama zetu na ameacha urithi wa kudumu wa mawazo na vitendo vya Qur’ani kwa ajili ya Ummah wa Kiislamu.”

Akirejelea urithi wa kudumu wa Ayatullah Sayyid Ali Khamenei katika nyanja ya Qur’ani Tukufu na wajibu wa jamii ya Qur’ani katika kuhifadhi urithi huu, alisema wengi wanaojihusisha na masuala ya Qur’ani huwa watu mashuhuri na vielelezo kwa jamii hiyo baada ya miaka mingi ya juhudi na mazoezi katika nyanja maalum.

“Watu wengi waliojitolea maisha yao kwa nyanja moja ya Qur’ani, kama vile qiraa (kusoma), kuhifadhi (hifdhi), kutafsiri, au kufasiri Qur’ani, hatimaye hujulikana kama msomaji, mhifadhi, mtafsiri, au mfasiri wa Qur’ani kupitia mapambano endelevu, na majina yao hubaki milele miongoni mwa wapenzi na wafuasi wa Qur’ani. Watu hawa huzingatiwa kama vielelezo vya vitendo na vinavyohamasisha, hasa kwa kizazi cha vijana. Kanuni hii haizuiliwi kwenye nyanja za kisayansi na kielimu za Qur’ani; hata msanii ambaye amefanya mazoezi kwa miaka mingi katika nyanja za sanaa za Kiislamu, kama vile khatt (hati za kiarabu/calligraphy) na uandishi wa Qur’ani, hatimaye huzingatiwa kama mwandishi na mpambaji wa Qur’ani, na hukuza ladha na vipaji vya wale wanaopenda sanaa ya Qur’ani.”

Salimi aliongeza, “Hoja ni kwamba baadhi ya watu wanapata jina la kudumu kutokana na shughuli zao katika tawi moja la Qur’ani. Kwa hiyo, utu ambao kila nyanja ya maisha yake, mawazo, mwenendo, na tabia yake imepakwa rangi na harufu ya Qur’ani, bila shaka uko kileleni mwa maadili ya Qur’ani na mifano ya mwenendo mwema.”

Akisisitiza kuwa mfano mkamilifu zaidi wa utu wa Qur’ani ni Mtume Muhammad (SAW), alisema, “Imesemwa kuhusu Mtume huyo kwamba asili yake ilikuwa Qur’ani, na kwa hakika, Mtume Mtukufu wa Uislamu (SAW) alikuwa Qur’ani inayotembea. Ikiwa tunataka kuanzisha utu katika zama za kisasa ambao, kwa kufuata mwenendo wa Qur’ani wa Mtume (SAW), ni dhihirisho la sifa hizi, ni lazima tumtaje Imam Shahidi wa Ummah, utu uliotumia miaka 86 ya maisha yake yenye baraka na wema katika njia ya kuipenda Qur’ani na kuonyesha katika nyanja ya mawazo na vitendo kwamba yeye ndiye kamanda wa kweli wa mstari wa mbele wa kusoma, kuhifadhi, kufahamiana na, na kutenda kwa mujibu wa Qur’ani.”

Salimi amemalizia kwa kusema, “Kwa hiyo, utu huu mkuu hauwezi kufupishwa katika mojawapo tu ya nyanja pana za utu wake wa Qur’ani, kwa sababu Kiongozi Shahidi ameacha kazi nyingi na baraka katika nyanja ya Qur’ani, mawazo na vitendo vya Qur’ani. Kila moja ya masalia haya inachukuliwa kuwa rasilimali ya thamani kwa jamii ya Qur’ani na lazima ihifadhiwe, ilindwe, na kuimarishwa kwa uangalifu ili ibaki kuwa kitovu cha tahadhari na wajibu wa jamii ya Kiislamu, na kila mmoja ajione kuwa anawajibika nayo.”

3498340

Habari zinazohusiana
captcha