IQNA

Iran yatangaza mipaka ya kutokea na kuingia kwa mazuwar wa kigeni wa Arbaeen

21:56 - July 15, 2026
Habari ID: 3482489
a
IQNA – Makao Makuu ya Ziyara ya Arbaeen nchini Iran, katika taarifa yake, yametangaza mipaka ya kutokea na kuingia kwa mazuwar wa kigeni wa Arbaeen ya Imam Hussein (AS) wanaosafiri kwenda Iraq kupitia Iran.

Taarifa hiyo imesisitiza kuwa raia wote wa kigeni walioidhinishwa wanaowasili kutoka nje ya nchi, pamoja na wale wanaoishi ndani ya Iran, wanapaswa kujisajili katika mfumo wa Samah.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mipaka ya kutokea na kuingia kwa raia wa kigeni na wageni wanaoishi nchini ni mipaka ya Shalamcheh na Chazzabeh katika mkoa wa Khuzestan, pamoja na mipaka ya Khosravi, Bashmaq na Tamarchin katika mikoa ya Kermanshah, Kurdistan na Azerbaijan Magharibi.

Arbaeen ni tukio adhimu la kidini linaloadhimishwa aghalabu na Waislamu wa madhehebu ya Shia siku ya arubaini baada ya Siku ya Ashura, ambayo ni kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imam Hussein (AS), mjukuu wa Mtume Muhammad (SAW) na Imamu wa tatu katika madhehebu ya Shia.

Hii ni miongoni mwa mijumuiko mikubwa zaidi za kila mwaka duniani, ambapo mamilioni ya Waislamu wa Kishia, sambamba na Waislamu wengi wa Kisunni na wafuasi wa dini nyingine, husafiri kwa miguu kuelekea Karbala kutoka miji mbalimbali ya Iraq na nchi jirani. Mwaka huu, siku ya Arubaini itaangukia tarehe 4 Agosti.

3498263

captcha