IQNA

Muhammad ni jina mashuhuri zaidi duniani

11:28 - November 10, 2013
Habari ID: 1314890
Jina la Mtume wa Uislamu, Muhammad (SAW) ndilo jina mashuhuri zaidi duniani. Hayo ni kwa mujibu wa uchunguzi wa gazeti la kila siku la Uhispania la ABC ambalo limeandika kuwa watu milioni 150 kote duniani wanatumia jina 'Muhammad.'
Gazeti hilo limeandika kuwa mbali na kuwa mashuhuri katika nchi za Kiislamu, jina Muhammad pia linatumika kwa wingi katika nchi zisizo za Kiislamu na ndilo jina mashuhuri zaidi la watoto katika baadhi ya maeneo ya Ufaransa. Jina Muhammad pia limetajwa kuwa la sita kwa umashuhuri nchini Uhispania na Uingereza.
Hivi karibuni pia, uchunguzi uliofanywa na Idara ya Biashara ya Milan nchini Italia na kuchapishwa Septemba 4, unaonyesha kuwa, 'Muhammad' ndio jina mashuhuri zaidi la wenye biashara ndogo ndogo mjini Milan.
 

1314431

captcha