IQNA

Tunisia yakanusha kumpa hifadhi shekhe wa fitna, Qardhawi

6:58 - April 13, 2014
Habari ID: 1394424
Waziri wa Mambo ya Nje wa Tunisia, amekadhibisha taarifa iliyosambazwa na vyombo vya habari kuhusiana na kuhamishiwa nchini humo ofisi ya Sheikh Yusuf Qardhawi, Mkuu wa Muungano wa Kimatiafa wa Maulama Waislamu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA,Ripoti iliyotolewa na idara ya habari na mawasiliano katika ikulu ya rais nchini Tunisia, jana ilimnukuu Monji Hamdi Waziri wa Mambo ya Nje akisema kuwa, habari za kuhamishwa nchini Tunisia ofisi ya Qardhawi, hazina ukweli wowote. Kwa mujibu wa ripo hiyo, Monji amemwambia Moncef Marzouki kuwa, katika safari ya hivi karibuni ya ujumbe wa serikali ya Tunisia ikiongozwa na Mehdi Jomaa, Waziri Mkuu wa Tunisia nchini Qatar na kukutana na kiongozi wa nchi hiyo Tamimbin Hamad al-Thani, hakukujadiliwa kwa namna yoyote habari kuhusu Qardhawi. Wakati huo huo afisa mmoja anayefanya kazi katika ofisi za Qardhawi alikadhibisha habari za kuhamishiwa nchini Tunisia ofisi ya sheikh huyo ambaye wengi wanamlaumu kwa kueneza fitna katika ulimwengu wa Kiislamu ikiwa ni pamoja na kutoa fatwa ya kuuawa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gadafi na kuchochea mauaji na umwagaji wa damu nchini Syria. Itakumbukwa kuwa, Naibu Mkuu wa Polisi na vikosi vya usalama wa wananchi vya Dubai mwanzoni mwa mwaka huu, alimtaja Sheikh Yusuf Qardhawi, Mkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Maulama wa Kiislamu kuwa, ni tishio kwa usalama wa eneo la Ghuba ya Uajemi na ulimwengu wa Kiislamu. Hivi karibuni baadhi ya vyombo vya habari vilieneza habari juu ya kuhamishiwa mjini Tunis kutoka Doha, ofisi za sheikh huyo.

1394210

Kishikizo: QARDHAWI FITNA tunisia doha
captcha