IQNA

Magaidi wa Kikristo waendelea kuwaangamiza vijana Waislamu CAR

14:29 - May 29, 2014
Habari ID: 1412082
Msemaji wa Jumuiya ya Waislamu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati amesema, wanamgambo wa Kikristo nchini humo wamewaua vijana watatu Waislamu na kukatakata viungo vyao vya mwili.

Othman Abakar, msemaji wa Jumuiya ya Waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ameongeza kuwa, vijana hao Waislamu wameuawa mjini Bangui wakati walipokuwa wakijitayarisha kuenda kutazama mechi ya mpira. Imearifiwa kuwa mechi hiyo ilikuwa baina ya vijana Waislamu na Wakristo kwa lengo la kuleta amani na maelewano baina ya Waislamu wa kundi la Seleka na wanagamabo wa Kikrsito wa kundi la Anti Balaka.

Msemaji huyo wa Waislamu ameongeza kuwa miili ya vijana hao waliokuwa wakaazi wa mtaa wa PK5 katika mji mkuu Bangui imezikwa katika msikiti mmoja mjini humo. Hayo yanajiri katika hali ambayo msemaji wa kundi la Kikristo la Anti-Balaka Sebastien Wenezoui amedai kulaani mauaji hayo na kuongeza kuwa vijana wengine 10 Waislamu wametekwa nyara katika tukio hilo. Amesema ukatili huo umetekelezwa na vijana wa Kikristo kutoka mtaa wa Boy-Rabe mjini Bangui. Hayo yanajiri katika hali ambayo siku ya Jumamosi kuliripotiwa mapigano makali baina ya wanajeshi wa Ufaransa na Waislamu watiifu kwa kundi la Seleka katika mji wa Bambari. Wanajeshi wa Ufaransa wajulikanao kama Sangaris wamekuwa wakiwashambulia Waislamu na kupuuza ugaidi unaofanywa na wanamgambo wa Kikristo.

1411178

captcha