IQNA

Kiongozi Muadhamu: Silaha za nyuklia ni dhidi ya ubinadamu

18:48 - June 09, 2014
Habari ID: 1415874
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa, silaha za nyuklia zinapingana kikamilifu na ubinadamu.

Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo leo mjini Tehran alipowahutubia wakuu, wakurugenzi na wahakiki wa Jihadi ya Vyuo Vikuu na kuongeza kuwa, sayansi ya nyuklia ni miongoni mwa mafanikio muhumi na yenye utata ya mwanadamu.
Kiongozi Muadhamu amesema, ingawa nyuklia ina umuhimu mkubwa, lakini inaweza kutumiwa katika kutengeneza silaha za maangamizi za atomiki, ambazo kwa asilimia 100 ziko dhidi ya ubinadamu. Ameongeza kuwa hivi sasa Iran ina uwezo wa kuzalishwa baadhi ya teknolojia za kisasa kutokana na kupiga hatua za maendeleo ya kisayansi, na ametoa wito wa kufanywa juhudi za kupatikana maendeleo katika teknolojia zinazoboresha maisha ya wanadamu kwa mujibu wa thamani za utu, badala ya zile ambazo zina madhara kwa mwanadamu.  
Katika upande mwingine, Ayatullah Khamenei amesema, Jihadi ya Vyuo Vikuu ni taasisi muhimu kwani chuo kikuu ni kituo cha elimu na maendeleo ya sayansi ya nchi, na kwamba kunafanyika jitihada za kujitolea katika kukabiliana na vikwazo na matatizo.

1415673

Kishikizo: khamenei nyuklia iran
captcha