IQNA

Taasisi ya Imam Hussein AS mashariki mwa Uganda

21:44 - July 23, 2014
Habari ID: 1432798
Taasisi ya Imam Hussein AS katika eneo la Bugiri Mashariki mwa Uganda ni moja ya vituo muhimu zaidi vya kuhubiri Uislamu na maarifa ya Ahul Bayt AS katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA Afrika Mashariki, eneo la Bugiri lina wakaazi takribani laki tano ambapo aghalabu ya watu hao ni Waislamu. Kati yao, Waislamu wa madhehebu ya Shia ni takribani 14,500. Mashia wa eneo hilo wako katika hali dhaifu kifedha na hivyo wako katika tabaka la wastani au la chini kijamii.
Taasisi ya Imam Hussein AS huko Bugiri iliasisiwa mwaka 2004 kwa ushirikiano wa Ayatullah Sadiq Shirazi, mmoja kati ya marajii wa kidini katika mji wa Qom nchini Iran kwa himaya ya baadhi ya wafuasi wake.
Taasisi hiyo inasimamiwa na Sheikh Ayub Muzzamil, msomi wa Kiislamu kutoka Uganda ambaye alihitimu katika Chuo cha Kidini cha Qom.
Taasisi hiyo inaendesha shughuli kadhaa za Kiislamu ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo ya Kiislamu, vipindi katika radio za kieneo, kusimamisha sala ya Ijumaa n.k.
1432367

captcha