IQNA

Rais Rouhani

Iran itaendelea kuwaunga mkono wanaodhulumiwa Ghaza

21:24 - August 06, 2014
Habari ID: 1436787
Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Waislamu katika Ukanda wa Ghaza hatimaye watapata ushindi dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kwamba Iran daima itasimama pamoja mataifa yote yanayodhulimiwa wakiwemo Wapalestina, Wairaqi na Wasyria.

Rais Rouhani ameyasema hayo leo Jumatano wakati akihutubia halaiki kubwa ya wananchi katika mji wa Shahr-e-Kord kaskazini magharibi mwa Iran. Ameongeza kuwa taifa la Iran liliunga mkono mapambano ya kishujaa ya Wapalestina wenye subira katika Ukanda wa Ghaza katika kipindi cha mwezi moja uliopita.

Rais Rouhani amesema, 'Waislamu wa Ghaza walisimama kidete na hatimaye wameibuka washindi mbele ya mabomu na makombora ya Wazayuni wenye kiu ya damu.' Rais wa Iran amesema si tu kuwa taifa adhimu, shujaa na la kimapambano la Iran daima limekuwa tayari kulinda maslahi yake bali pia linatetea maslahi ya Waislamu na wanaodhulumiwa kote duniani.

Kwingineko katika hotuba yake Rais Rouhani amesema taifa la Iran litaendelea na sera zake za "ulaini wa kishujaa" katika kukabiliana na madola ya Magharibi. Amesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katu haitasalimu amri mbele ya madola makubwa ya kibeberu. Ameongeza kuwa Iran inatumia mantiki na ufahamu sahihi katika kutetea haki za taifa hili.

1436513

captcha