IQNA

Wapalestina washangilia ushindi katika vita na Israel

16:59 - August 27, 2014
Habari ID: 1443936
Maelfu ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza wameendelea kusherehekea kufikiwa makubaliano ya muda mrefu kuhusu usitishaji mapigano kati ya makundi ya muqawama na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Wapalestina wamemiminika katika barabara wakipiga vigelegele na vifijo kusherehekea ushindi huo dhidi ya Wazayuni. Harakati ya Hamas imesema kuwa, makubaliano hayo ni ushindi kwa Wapalestina na kutoa wito wa kufanywa maandamano ya kusherekea, huko Ukingo wa Magharibi pia unaokaliwa kwa  mabavu.
Ismail Haniya Naibu Mkuu wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas,  amesema mapatano hayo ni ushindi mkubwa kwa taifa la Palestina.
Katika upande mwingine harakati ya Jihadul Islami ya Palestina imesema, suala la silaha za wapiganaji wa muqawama halikujumuishwa katika ajenda ya mazungumzo na Israel.  Ramadhani Abdallah Shalah, Katibu Mkuu wa harakati hiyo ameeleza kuwa, kupokonywa silaha makundi ya muqawama ya Palestina halikuwa takwa katika mazungumzo na utawala wa Kizayuni kwa ajili ya usitishaji vita wa muda mrefu.
Mapatano ya kusitisha vita kwa muda mrefu, kuondolewa mzingiro wa Israel dhidi ya Ghaza na dhamana kuhusu kutekelezwa matakwa na mahitaji ya Palestina ni kati ya mambo yaliyoafikiwa na pande mbili.
Makundi ya wanamapambano wa Palestina na maafisa wa utawala haramu wa Israel wamefikia mapatano ya usitishwaji vita wa muda mrefu katika Ukanda wa Ghaza.Wapalestina wamekuwa wakisisitiza kuwa sharti lao la kukubali usitishwaji vita na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kuondoa mzingiro kikamilifu dhidi ya Ukanda wa Ghaza. Tokea Israel ianzishe mashambulio yake ya kinyama dhidi ya Ghaza Julai 8 hadi sasa, Wapalestina karibu 2, 200 wameuawa shahidi wakiwemo watoto 570 na wengine zaidi ya elfu 10 wamejeruhiwa.

1443576

captcha