IQNA

Maqari 1800 washiriki mashindano ya Qur'ani ya Pakistan

11:31 - September 21, 2014
Habari ID: 1452131
Mashindano ya kuhifadhi Qur'ani yaliyowashirikisha mahafidh 1800 wa Qur'ani Tukufu yamefanyika katika mji wa Islamabad nchini Pakistan.

Mashindano hayo yamefanyika kwa ushirikiano wa Jumuiya ya Kimataifa ya Hifdhi ya Qur'ani Tukufu na ofisi ya Jumuiya ya Kimataifa ya Uislamu nchini Pakistan yakiwashirikisha maqari 1800 wa kike na kiume.
Sherehe za kufungua mashindano hayo zimehudhuriwa na Rais Mamnoon Hussain wa Pakistan, balozi wa Saudi Arabia mjini Islamabad Abdul Aziz bin Ibrahim na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Islamabad, Ahmad Yusuf Darwish.
Mashindano hayo yalijumuisha vitengo vya hifdhi ya Qur'ani na kiraa mbalimbali, hifdhi ya Qur'ani na kitabu cha Riyadhu Swalihin, hifdhi ya Qur'ani na kitabu cha Muqaddimatul Jazariyyah, hifdhi ya Qur'ani na maana ya maneno yake na hifdhi ya Qur'ani makhsusi kwa watoto wadogo. AIR  1451810

captcha