IQNA

Kikao cha OIC chafanyika Jeddah kuhimiza hatua za kumaliza mauaji ya kimbari Gaza

9:26 - August 26, 2025
Habari ID: 3481136
IQNA – Mkutano wa dharura wa mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Shirika la Ushirikiano la Kiislamu (OIC) ulianza Jumatatu mjini Jeddah, Saudi Arabia, ambapo washiriki wamesisitiza umuhimu wa hatua ya pamoja kusaidia Gaza na Palestina.

Lengo la mkutano huu ni kuchunguza njia za kukabiliana na mashambulizi ya utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, amesema katika hotuba yake kwamba kinachohitajika na watu wa Palestina ni hatua ya pamoja.

Fidan ameongeza kuwa utawala wa Israel unapaswa kushinikizwa kwa nguvu na kwa ushirikiano ili kupata suluhisho la kudumu la suala la Palestina.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Saudi Arabia, Faisal bin Farhan, pia amezungumza katika mkutano huo Jumatatu na kusema kwamba utawala wa Kizayuni unaleta tishio kwa amani na usalama wa kimataifa.

Amesisitiza kuwa jamii ya kimataifa lazima imalize uhalifu unaofanywa na utawala wa Kizayuni na kuupinga.

Waziri bin Farhan ameisisitiza haki ya Wapalestina ya kuanzisha taifa lao huru.  Aidha ameunga mkono juhudi za Misri na Qatar za kufikia mapatano ya kusitisha mapigano Gaza, huku akilaani matamshi ya waziri mkuu wa Israel kuhusu mpango wa "Israeli Kubwa."

Mwakilishi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa, Riyad Mansour, pia amezungumza katika mkutano huo na amesisitiza kwamba matamshi ya viongozi wa Israeli kuhusu kuanzisha "Israeli Kubwa" kutoka Mto Nile hadi Mto Euphrates yanalaaniwa kabisa, na kusema kuwa nchi za Kiislamu lazima zishirikiane zote kutokomeza itikadi ya kujitania Israel.

Mansour aliongeza kwamba kushindwa kwa jamii ya kimataifa kuwawajibisha viongozi wa Israeli kumewafanya kumewafanya wapate kiburi zaidi.

Kauli ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, pia alizungumza katika mkutano wa OIC. Amelaani mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina huko Gaza na kusisitiza haja ya hatua za kukabiliana na utawala wa Kizayuni.  Ametoa wito wa kuchukuliwa hatua madhubuti za kimataifa kukomesha mauaji ya halaiki ya Israel yanayoendelea huko Gaza, akisema kuwa nchi zote zinapaswa kusimama upande sahihi wa historia ambao "hautasamehe" ucheleweshaji wowote zaidi wa kupunguza mateso ya watu wa Palestina.

Mkutano wa Dharura wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa OIC umefanyika kufuatia ombi la Iran, ambalo lilitumwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Abbas Araghchi kwa Katibu Mkuu wa OIC, mnamo tarehe 6 Agosti.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameongeza kuwa: "Tukumbuke kuwa maafa ya Gaza hayawahusu Waislamu pekee. Ni mtihani kwa dhamiri ya kimataifa. Kwa hivyo, tunatoa wito kwa mataifa yote, bila kujali dini au jiografia, kusimama upande wa ubinadamu, haki, na heshima, ambayo ni upande sahihi wa historia," amesema Araghchi na kusisitiza kuwa, "Historia haitasamehe usuasuaji. Gaza haiwezi kusubiri. Wakati wa kuchukua hatua ni sasa."

Sayyid Araghchi ameeleza bayana kuwa: Leo, tumekusanyika wakati ambapo Gaza inasimama mbele ya dhamiri yetu kama kioo kinachoogofya. Kinachojitokeza mbele ya macho yetu ni uharibifu uliopangwa wa watu waliozingirwa, na utawala dhalimu wa ubaguzi wa rangi ambao unafanya unalotaka bila kubebeshwa dhima au kuadhibiwa.

Ameeleza kuwa, watu wa Gaza wanauawa kwa utaratibu maalum, maeneo ya makazi yameharibiwa kabisa; hospitali zimegeuzwa kuwa makaburi; na watoto wamenasa katika njaa kali; huu ukiwa ukiukaji wa wazi wa kila kiwango cha binadamu. Hivi sivyo vita vya kawaida. Ni adhabu ya pamoja, sera ya kutawala, na mashambulio ambayo yana ishara zote za mauaji ya kimbari.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria Hadithi ya Mtume Muhammad (SAW) alipotufundisha kwamba, Umma wa Kiislamu ni kama mwili na roho moja. "Leo, mwili huu una maumivu na umerowa kwa damu huko Gaza. Kukaa kimya ni kujiumiza wenyewe, na hatua ya ujasiri ndiyo njia ya uponyaji," amefafanua mwanadiplomasia huyo mkuu wa Iran.

Hali kadhalika, Waziri Araghchi amezitolea wito nchi za Kiislamu kuchukua hatua za pamoja kukabiliana na ajenda ya kujitanua ya Israel katika eneo la Asia Magharibi kupitia kampeni ya 'Israel Kubwa Zaidi'.

Ameongeza kuwa, ili kuanzisha mchakato wa amani na kuhakikisha vikosi vamizi vya Israel vinaondoka kikamilifu kutoka kila shibri ya Gaza, lazima tujitolee kuhamasisha utumiaji wa zana zote za kisiasa, kiuchumi na kisheria ikiwa ni pamoja na vikwazo, ususiaji wa bidhaa, na mashinikizo ya kimataifa yaliyoratibiwa.

3494383

Habari zinazohusiana
Kishikizo: oic gaza iran israel
captcha