IQNA

Imarati yayashambulia vikali makundi ya kitakfiri

0:03 - September 30, 2014
Habari ID: 1455492
Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) ameyashambulia vikali makundi ya kigaidi na kitakfiri katika eneo la Mashariki ya Kati akisema kuwa makundi hayo yanaonyesha picha mbaya kwa dini tukufu ya Kiislamu.

Sheikh Abdullah bin Zayed Aal Nahyan amesema hayo wakati akihutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York Marekani na kuongeza kuwa, vitendo vya makundi hayo ya kigaidi kama vile kuua watu kiholela, kuua watu kwa umati, kuteka nyara watu, kuwanyanyasa na kuwakandamiza vibaya wanawake na watoto wadogo wasio na hatia ni jinai, na kwamba Imarati inalaani vikali jinai hizo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu vile vile amesema, uhalifu wa kutisha unaofanywa na makundi hayo unakinzana kikamilifu na mafundisho ya Uislamu na kwamba makundi hayo yanafanya kosa kubwa yanapobeba bendera ya dini ili kuhalilalisha jinai zao. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Imarati pia amesema, nchi yake inalaani mbinu za kudhulma zinazotumiwa na makundi hayo yaliyojipachika jina la Uislamu kwani jinai na uhalifu wa makundi hayo unapingana kikamilifu na misimamo ya wastani na kuishi na watu wengine kwa usalama na amani.../mh

1454929

captcha