Akizungumza kwenye kongamano lililoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu kwenye Msikiti Mkuu wa Rome lenye mada 'Ugaidi hapana, Uislamu dini ya amani', Spika Laura Boldrini amesisitiza kwamba kundi la kigaidi la Daesh siyo tishio pekee kwa nchi za Magharibi bali ni tishio pia kwa ulimwengu mzima na hasa kwa Waislamu. Spika wa Bunge la Italia amesema kuwa, wananchi wa Italia wanaamini kwamba, Uislamu siyo ule unaozungumzwa na kutekelezwa na magaidi wa Daesh, bali Uislamu ni dini ya amani na upendo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Daesh ni moja kati ya makundi makuu ya kigaidi ambayo yanapata uungaji mkono wa kifedha na kisilaha na nchi za Magharibi na hasa Marekani, Uingereza na Ufaransa wakisaidiwa na watawala wa nchi za Kiarabu kama vile Saudi Arabia na Qatar kwa lengo la kuleta ghasia na machafuko na hatimaye kuziangusha serikali halali za Syria na Iraq.../mh