Sheikh Ahmed Mohamed Ahmed El-Tayeb ameashiria mauaji na mauaji ya kimbari duniani, vikiwemo vita vya mauaji ya kimbari vya utawala ghasibu wa Israel katika Ukanda wa Gaza na kusema dunia inakabiliwa na ukosefu wa shauku na azma ya kuleta amani.
Hii imefanya amani kuwa nia isiyoweza kufikiwa, amesema hivi karibuni.
Sheikh El-Tayeb ameyasema hayo katika mkutano na Syafruddin Kambo, mwenyekiti wa Wakfu wa Amani Duniani.
Amesema kutokana na uchokozi na ukatili wa kila siku, dhana ya amani imekuwa ikidhoofishwa.
Matakwa yetu makubwa katika hali ya sasa ni kupatikana amani katika eneo na dunia na kukomesha mateso ya taifa la Palestina ili waweze kurejesha haki zao na kuanzisha nchi yao huru na kuishi kwa amani na usalama kama mataifa mengine, Sheikh El-Tayeb amesema.
Mkutano huo umekuja wakati ambapo Misri inashiriki katika juhudi kubwa za kidiplomasia kwa ajili ya kumaliza vita vya Israel dhidi ya Gaza.
Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel lilianza mashambulizi makali huko Gaza mwezi Oktoba mwaka jana.
Zaidi ya Wapalestina 43,300 wameuawa tangu wakati huo, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, na zaidi ya 100,000 wamejeruhiwa, kulingana na mamlaka ya afya ya eneo hilo.
Mashambulizi hayo ya Israel yamewafanya takriban wakazi wote wa eneo hilo kuwa wakimbizi kutokana na mzingiro unaoendelea ambao umesababisha uhaba mkubwa wa chakula, maji safi na dawa.
Israel sasa nakabiliwa na kesi ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki kwa vita vyake vya kikatili dhidi ya Gaza.
3490551