IQNA

Mashia Misri wamualika Sheikh wa al-Azhar kushiriki kwenye Ashura

16:02 - October 31, 2014
Habari ID: 1465815
Waislamu wa Kishia nchini Misri wamemwalika Sheikh Mkuu wa al-Azhar kuhudhuria shughuli ya maombolezo ya Ashura ya kukumbuka kuuawa shahidi Imam Hussein mjukuu wa Mtume Muhammad SAW.

Sayyid Twahir al-hashimi, mwanaharakati wa Kiislamu wa madhehebu ya Kishia nchini humo na jumbe wa Jumuiya ya Kimataifa ya Ahlul-Bayt AS amemtaka Sheikh Ahmad at-Twayyib, Sheikh Mkuu wa al-Azhar kushiriki katika maombolezo hayo ya mwaka huu yatakayofanyika katika msikiti wa Imam Hussin AS mjini Cairo. Mbali na Sheikh al-Hashimi kumwalika sheikh huyo wa al-Azhar kuhudhuria shughuli hiyo, amemtaka pia kutoa mawaidha katika marasimu hayo. Kwa upande wake, Shauqi Abdul Latif, Naibu Waziri wa Waqfu wa Misri pia ametoa ujumbe akisema kuwa, kuwapenda Ahlul-Bayti wa Mtume, ni wajibu kwa Waislamu wote hasa kwa kuzingatia kwamba hata Qur’an Tukufu imewatakasa na kuinua daraja ya watu hao wa Nyumba ya Mtume (saw). Amesema kuwa, Wamisri wanawatukuza Ahlul-Bayt wa Matume na kwamba kuwapenda ni kumpenda Mtume wa Uislamu. Katika siku za Muharram, Waislamu wa Kishia nchini Misri, kama walivyo Waislamu wa nchi nyngine, hukumbuka kuuawa shahidi kiongozi wa mashahidi, Imam Hussein (as) katika maeneo tofauti ya Misri, ukiwemo msikiti wa Imam Hussein mjini Cairo.../mh

1465488

captcha