Abdul Hay Azab Mkuu wa Chuo Kikuu cha al Azhar amesema kuwa, Sheikh Ahmad Karima amepigwa marufuku kufundisha Chuo Kikuu cha al Azhar kwa muda wa miezi mitatu, na baada ya kumaliza adhabu hiyo atafunguliwa mashtaka mahakamani kwa kosa la kuitembelea Iran. Chuo Kikuu cha al Azhar kimevitaka vyombo vya mahakama kuchunguza suala hilo na ikiwezekana kutoa adhabu kali dhidi ya Sheikh Ahmad Karima ikiwemo ya kumpiga marufuku moja kwa moja kufundisha na kumvua hadhi yake ya uwanazuoni. Katika kujibu ukosoaji ulioelekezwa dhidi yake, Sheikh Ahmad Karima ameeleza kwamba, asingeliizuru Iran, kama serikali ya Misri ingelitangaza kinagaubaga kwamba, Iran ni nchi adui kwa taifa la Misri.../mh