Kituo cha habari cha Brunei Times kimeripoti kuwa duru ya kwanza ya mashindano hayo ilifanyika jana kwa kuwakutanisha Waislamu wapya katika mkoa wa Tutang nchini humo.
Mashindano kama hayo ya utangulizi yatafanyika katika mikoa yote minne ya Brunei na wale watakaopata nafasi za juu watachuana katika mashindano ya kitaifa yatakayofanyika katika mji mkuu wa Brunei, Bandar Seri Begawan, tarehe 30 mwezi huu.
Mashindano hayo yaliyotayarishwa na Kituo cha Ulinganiaji wa Kiislamu cha Brunei yanafanyika kwa lengo la kuwahamasisha Waislamu wapya kusoma Qur'ani Tukufu.
Haji Ja'far ambaye ni miongoni mwa viongozi wa kituo hicho amesema lengo jingine la mashindano hayo ni kuimarisha mahusiano baina ya Waislamu.