IQNA

Chuo cha taaluma ya juu cha Qurani kuanzishwa nchini Saudi Arabia

13:56 - November 02, 2008
Habari ID: 1703262
Naibu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhi Qurani katika eneo la mashariki mwa Saudi Arabia amesema kuwa akademia ya taaluma ya juu ya kuhifadhi na kusoma Qurani Tukufu itaanzishwa hivi karibuni katika mji wa Dammam mashariki mwa Saudi Arabia.
Gazeti la al Riyadh la Saudi Arabia limemnukuu Yusuf al Afaliq akisema kuwa lengo la kuanzishwa chuo hicho cha taaluma ya juu ya Qurani ni kutayarisha masomo ya juu ya kuhifadhi, kusoma na tajwidi haswa kwa watu wa eneo la mashariki mwa nchi hiyo.
Al Afaliq amesema, mbali na akademia hiyo, kutaanzishwa kituo maalumu kwa ajili ya masomo ya kuhifadhi Qurani na misaada ya kibinadamu katika mji wa Dammam.
Yusuf al Afaliq amesema kuwa duru ya sita ya masomo ya kuhifadhi Qurani Tukufu kwa watu wa eneo la mashariki mwa Saudi Arabia ilifanyika tarehe kumi hadi 30 mwezi uliopita wa Oktoba chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Jumuiya ya Kuhifadhi Qurani mashariki mwa Saudi Arabia katika msikiti mtakatifu wa Makka. 313759



captcha