Kwa mujibu wa ukurasa wa intaneti wa gazeti la Birmingham Mail , walioandaa programu hiyo wamesema, lengo ni kuuarifisha Uislamu halisi ili kukabiliana na propaganda chafu na zisizo za kweli ambazo zimekuwa zikienezwa dhidi ya jamii ya Waislamu. Kwa mujibu wa Alan Rudge Mkuu wa Baraza la Mji wa Birmingham aliyetangaza rasmi wiki hiyo ya kuufahamu Uislamu, programu hiyo itajumuisha maonyesho ya filamu, mihadhara na usomaji mashairi. Ameongeza kuwa, kuandaliwa wiki hiyo kutakuwa fursa nzuri ya mazungumzo huru na ya kweli.
Itakumbukwa kuwa zaidi ya asilimia 2.7 (Millioni 1.6) ya watu milioni 60 wa Uingereza wanajitambulisha rasmi kama Waislamu. 317128