IQNA

Darul Quran Maryam(S) : Kituo cha harakati za Quran huko Kyrgyzstan

16:04 - November 10, 2008
Habari ID: 1706756
Taaisi ya Darul Quran Maryam (S) katika mkoa wa Jalalabad Kyrgyzstan inatoa mafunzo ya tajwid na kuhifadhi Quran Tukufu kwa wanawake wa eneo hilo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa Shirika la Habari la Quran IQNA huko Kyrgyzstan, darsa za Quran katika taasisi hiyo zina wanafunzi 50 ambao wote ni wanawake walio kati ya umri wa miaka 14-20.
Huko nyuma eneo la kusini mwa Kyrgyzstan lilikuwa ni mkoa mmoja uliojulikana kwa jina la Osh. Hivi sasa eneo hilo limegawanywa na kuwa na mikoa mitatu inayojumuisha Osh, Jalaabad na Batken. Pamoja na mabadiliko hayo kuna uhusiano wa karibu kati ya maeneo hayo yote. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, mkoa wa Jalalabad una wakaazi wapatao 71 elfu.
Kyrgyzstan ni nchi ya Kiislamu iliyo katika eneo la Asia ya Kati. Inapakana na Kazakhstan upande wa kaskazini, Uzbekistan upande wa magharibi, Tajikistan upande wa kusini magharibi na China upande wa Mashariki. Nchi hiyo ina jamii ya watu zaidi ya milioni tano.316861
captcha