IQNA

16:55 - August 16, 2026
Habari ID: 3482633

Washiriki wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Makka wapata zawadi za fedha

IQNA – Washindi na washiriki katika mashindano ya 46 ya Kimataifa ya Qur’ani ya Mfalme Abdulaziz, yaliyofikia tamati Makka mapema wiki hii, wametunukiwa zawadi za fedha mwishoni mwa hafla hiyo ya Qur’ani.

a

Wizara ya Masuala ya Kiislamu, Dawah na Uongozi ya Saudi Arabia, kupitia Sekretarieti Kuu ya Mashindano ya Kimataifa ya Mfalme Abdulaziz ya Kuhifadhi, Kusoma na Kufasiri Qur’ani Tukufu, imewapatia washiriki katika toleo la 46 la mashindano hayo zawadi za kifedha za Riyal 5,000 kila mmoja, jumla ikiwa zaidi ya Riyal milioni 1.5, ili kutambua juhudi zao na kuhamasisha uendelevu wa ari yao kwa Qur’ani Tukufu.

Toleo hilo la 46 lilishirikisha washindani 334, wanaume kwa wanawake, wakiiwakilisha nchi 133, waliokabiliana katika makundi matano ya Qur’ani. Thamani ya jumla ya zawadi kwa washindi 50 waliotajwa ilifikia Riyal 10,260,000.

Tuzo hizo ni sehemu ya uangalizi ambao wizara hiyo, ikiwa msimamizi mkuu wa mashindano ya Qur’ani, huutoa kwa washiriki wa kiume na wa kike.

Wizara hiyo inasema imejizatiti kutoa msaada wa kina kuanzia wakati washiriki wanapowasili nchini humo, kupitia hatua za awali na za mwisho za kufuzu, pamoja na programu zinazoambatana na mashindano hayo, jambo linalodhihirisha umuhimu unaotolewa kwa mashindano hayo na dhamira ya kutumikia Kitabu Kitukufu cha Mwenyezi Mungu.

/3498658

captcha