IQNA

Arbaeen: Tukio adhimu linalovuka mipaka ya ibada ya kawaida

18:09 - August 04, 2026
Habari ID: 3482586
IQNA – Matembezi ya Arbaeen si tukio la kitamaduni pekee wala ibada ya kawaida, bali ni dhihirisho la falsafa ya kina ya ustaarabu na utu inayoyaita nyoyo za watu huru duniani kuelekea kwenye ukweli, uadilifu, na uhuru.

Haya ni kwa mujibu wa makala iliyoandikwa na msomi wa Kiirani, Profesa Mohammad Fanaei Eshkevari.

Makala hiyo inasema:

Matembezi makubwa na Ziyara ya Arbaeen ya Imam Hussein (Amani iwe juu yake-AS-) nchini Iraq ni tukio kubwa la kiutamaduni, kijamii, na kisiasa na kidini ambalo linachukuliwa kuwa la kipekee katika ulimwengu wa sasa kwa mitazamo mbalimbali. Harakati hii ya mamilioni ya watu si tukio la kitamaduni pekee au ibada yenye mipaka, bali ni dhihirisho la falsafa ya kina ya ustaarabu na utu inayoyaita nyoyo za watu huru duniani kuelekea kwenye ukweli, uadilifu, na uhuru.

Kufufua Mwamko na Kuihuisha Ujumbe wa Sayyid al-Shohada (Bwana wa Mashahidi, yaani Imam Hussein -AS-)

Falsafa muhimu zaidi ya Arbaeen ni kuhifadhi na kuendeleza ujumbe wa Ashura. Ashura si tukio la kihistoria pekee; ni shule endelevu ya kupambana na dhulma, kutetea heshima ya binadamu, na kulinda dini ya Mwenyezi Mungu. Arbaeen ni mwendelezo wa harakati ya kufikisha ujumbe wa Ashura ambayo ilianzishwa na Bibi Zaynab al-Kubra (AS) na Imam Sajjad (AS),utume ambao haukuruhusu damu ya mashahidi wa Karbala kupotea kwenye vumbi la upotoshaji na kusahaulika.

Dhihirisho la Kivitendo la Kaulimbiu ya “Laiti Tungelikuwa Pamoja Nanyi” (Ya Laytana Kunna Ma’ak)

Mazuwar wa Arbaeen hawaonyeshi mapenzi kwa maneno tu; wanaonyesha utiifu wao kwa hatua zao. Kutembea makumi na wakati mwingine mamia ya kilomita kwa miguu, kuvumilia joto, uchovu, na changamoto za safari ni tamko la kivitendo la utayari wa kuunga mkono shule ya Husayni.

Uaminifu wa Pamoja na Onyesho la Azimio la Ummah

Safari ya Arbaeen ni njia ya kiroho ya mtu binafsi na harakati ya pamoja. Ingawa ni uzoefu wa kiroho kwa watu binafsi, pia ni onyesho kuu la azimio la pamoja la Ummah wa Kiislamu. Uwepo wa mamilioni ya watu pamoja ni dhihirisho la mshikamano miongoni mwa wafuasi wa kweli na wanaotafuta haki kote ulimwenguni.

Mshikamano Usio na Kifani na Ukarimu

Arbaeen ni jukwaa ambapo maadili ya juu zaidi ya kibinadamu na kiroho yanadhihirika. Katika umati mkubwa, kitu kinachojitokeza zaidi ni utulivu, nidhamu, uungwana, ushirikiano, na hisia ya udugu wa kweli.

Kafara ya Kifedha na Dhihirisho la Utamaduni wa Huduma

Moja ya maajabu ya Arbaeen ni ukarimu wa watu wa Iraq na wahudumu katika ‘Mawkib’ (vituo vya huduma bila malipo). Wanaweka nyumba zao, mali zao, muda wao, na nguvu zao katika huduma ya Mazuwar bila kutarajia malipo yoyote, wakiona kuwa huduma kwa mazuwar wa Imam Hussein (AS) ni heshima na tunu ya kiroho.

/3498528

captcha