IQNA

Mashindano ya Usomaji wa Qur’ani nchini Qatar yanalenga kugundua vipaji vya kipekee

17:19 - August 04, 2026
Habari ID: 3482583
q
IQNA – Taasisi ya Kijiji cha Utamaduni (Katara) nchini Qatar imefungua milango ya maombi kwa ajili ya Toleo la 10 la Tuzo ya Usomaji wa Qur’ani Tukufu. Mashindano hayo ya Qur’ani yanafanyika chini ya kauli mbiu: “Kuimarisha Sauti za Usomaji Mwema”.

Katika taarifa yake, Katara imesema kuwa maombi yalianza kupokelewa tarehe 3 Agosti na yatafungwa tarehe 30 Septemba. Tuzo hii inalenga kugundua na kuhamasisha vipaji bora katika usomaji wa Qur’ani, kubainisha sauti nzuri zaidi za usomaji, na kuwatambua wasomaji mahiri kwa kuzingatia kanuni sahihi za Tajweed.

Jopo la majaji linaundwa na wataalamu watatu wa usomaji wa Qur’ani na Tajweed, pamoja na wataalamu wengine watatu waliobobea katika elimu ya Maqamat, ubora wa sauti, na mahadhi. Kama sehemu ya tuzo hiyo, Katara itatayarisha na kutoa rekodi kamili ya sauti ya Qur’ani Tukufu itakayosomwa na mshindi wa kwanza katika studio za Katara.

Jumla ya zawadi iliyotengwa ni Qatari Riyal 800,000, ambapo mshindi wa kwanza atapokea Qatari Riyal 500,000, mshindi wa pili atapata Qatari Riyal 200,000, na mshindi wa tatu atapata Qatari Riyal 100,000. Idara Kuu ya Wakfu katika Wizara ya Awqaf (Wakfu) na Masuala ya Kiislamu ya Qatar imekuwa mfadhili rasmi wa tuzo hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 2017.

3498527

Habari zinazohusiana
captcha