IQNA

Ujumbe wa Wahyi / 4

Ukamilifu na Ujumuishi wa Qur’ani Tukufu

15:13 - August 03, 2026
Habari ID: 3482577
IQNA-Qur’ani Tukufu, kitabu cha mwongozo na mwamko wa mwanadamu, katika aya zake inawasilisha ujumbe ulio wazi na wenye kutoa mwanga kwa nyakati zote na kwa wanadamu wote; jumbe hizi zinajumuisha kila kitu kuanzia utunzaji wa imani na maadili ya mtu binafsi, hadi kusimama imara katika dhiki, kuwa na matumaini kwa rehema za Mwenyezi Mungu, uwajibikaji katika jamii, kuepuka kughafilika, na kusonga mbele katika njia ya haki.

Mfululizo huu wa “Ujumbe wa Wahyi,” kwa kuchagua aya zenye mada maalum, unajitahidi kujenga daraja dhahiri kati ya dhana kuu za wahyi na maisha ya sasa ya wasomaji, huku ukiweka kila aya mbele ya msomaji kama ujumbe wenye kuhamasisha, wenye kutoa nafasi ya kutafakari, na wenye manufaa ya kiutendaji. Aya hizi zinachapishwa kwa lengo la kukuza utamaduni wa tadabburi (kutafakari kwa kina) katika Qur’ani, kuimarisha basira (bainisho/ufahamu) na matumaini, na kutoa mwanga katika nyanja za maisha ya mtu binafsi na ya kijamii, ili kuandaa mazingira ya kupata mwamko zaidi, kurekebisha tabia, na kusonga mbele katika njia ya uongofu wa Mwenyezi Mungu.

 

 

وَنَزَّلْنَا عَلَيْكَ الْكِتَابَ تِبْيَانًا لِكُلِّ شَيْءٍ

Na tumekuteremshia Kitabu hiki kinacho bainisha kila kitu

Sehemu ya aya ya 89 ya Sura Nahl

جامعیتِ قرآن کریم

captcha