IQNA

Mazuwar wa Arbaeen watoa wito wa kulipiza kisasi cha amu ya Kiongozi Shahidi

17:12 - August 04, 2026
Habari ID: 3482582
a
IQNA – Kongamano la Mazuwar wa Arbaeen likitoa wito wa kulipiza kisasi cha damu ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah SayyidAli Khamenei, limefanyika barabarani kati ya Najaf na Karbala, nchini Iraq. Tukio hili lameshuhudia mahudhurio makubwa ya jamii ya wapenzi wa Qur’ani kutoka Iran, Iraq, na kundi la Mazuwar kutoka mataifa mengine ya Kiislamu.

Katika mkusanyiko huu, wajumbe wa jumuiya ya Qur’ani ya Iran, pamoja na Mazuwar wengine, wamebeba bendera zenye ujumbe wa “Ya Litharat al-Hussein (AS)” na kusisitiza umuhimu wa kuendeleza njia ya haki, kutafuta uadilifu, na kukabiliana na dhulma kwa kauli mbiu zenye kuleta umoja. Washiriki wa harakati hii ya kiroho walitembea katika njia iliyo kati ya nguzo namba 1080 hadi 1090 kwenye barabara ya Najaf-Karbala, katika hali iliyojaa hamasa ya Husseini na nuru ya kiroho.

Shughuli hiyo ilijumuisha usomaji wa aya za Qur'ani Tukufu, ukumbusho wa Ahl-ul-Bayt (AS), na kuhuisha agano na tunu za Ashura. Ilidhihirisha mshikamano wa Ummah wa Kiislamu katika kongamano kubwa zaidi la kidini duniani. Waliohudhuria mkusanyiko huu wameitazama matembezi ya Arbaeen kama dhihirisho la mwendelezo wa harakati ya Ashura na alama ya upinzani dhidi ya dhulma, na kusisitiza kuwa utamaduni wa Ashura ni mwongozo kwa mataifa huru duniani katika safari ya kufikia haki na heshima ya mwanadamu.

Pembezoni mwa mkusanyiko huu, wanaharakati na viongozi wa Qur’ani, wakirejelea uhusiano wa kina kati ya utamaduni wa Qur’ani na shule ya Imam Hussein (AS), wameelezea Arbaeen kama fursa ya kueneza mafundisho ya Mwenyezi Mungu, kuimarisha umoja wa Ummah wa Kiislamu, na kuhuisha agano na maadili ya Qur’ani na Ahl-ul-Bayt (AS).

3498526

Habari zinazohusiana
captcha