Kwa muibu wa Shirika la Habari za Qur’ani la Kimataifa IQNA, waliohutubu katika hafla hiyo walizungumzia athari za fikra za Imam Ridha (as) katika kupambana na kufri. Waliozungumza katika hafla hiyo ni pamoja na Sheikh Jibril, Mkuu wa Kituo cha Ahlul Beit (as) ambaye pia ni mkuu wa Baraza la Mji wa Livingstone na Sheikh Ali Banda Mkuu wa Jumuiya ya Maulamaa na pia Baraza Kuu la Waislamu wa Zambia aliyezungumzia udharura wa kujua na kufuata mafundisho ya Imam Ridha (as). Katika hafla hiyo Hujjatul Islam wal Muslimeen Muhammad Asadi Muwahhid, Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Zambia alihutubia hafla hiyo kwa kuzungumzia nafasi ya Imam Ridha (as) katika kupambana na bidaa na kuenezwa upotofu katika zama za utawala wa Bani Abbas. Alisema upotofu huo ulizushwa kwa kutarjumiwa baadhi ya vitabu vya kifalsafa vya Wagiriki, jambo ambalo Imam Ridha alikabiliana nalo vilivyo kupitia hotuba zake za kimantiki na zilizokubaliwa na wengi waliohudhuria vikao vyake. Aliashiria pia mijada muhimu ya kielimu iliyokuwa ikifanyika katika darsa za mtukufu huyo jambo ambalo lililoondoa upotofu na imani zisizo na msingi zilizokuwa zikienezwa katika zama hizo kuhusiana na masuala ya itikadi, upwekeshaji Mwenyezi Mungu, Utume na Uimamu. Sherehe nyingine za kuadhimishwa uzawa wa Imam Mahdi zilifanyika katika miji mingine ya nchi hiyo. 318242