IQNA

Kuanza mashindano ya Quran Tukufu Qatar

14:28 - November 11, 2008
Habari ID: 1707121
Duru ya tatu ya Mashindano ya kuhifadhi, kusoma na kutafsiri Quran yameanza Jumanne asubuhi katika makao ya kuhifadhi Quran katika mji mkuu wa Qatar, Doha.
Kwa mujibu wa gazeti la kila siku la Qatar la Ar-Rabita, Khalid Bin Mohammad bin Ghanim Al Thani mkuu wa kamati iliyoandaa mashindano hayo amesema kuwa: 'Mashindano ya Quran ya "Sheikh Ghanim" yanafanyika kwa usimamizi wa Wizara ya Wakfu na Masuala ya Kiislamu ya Qatar. Upande wa wanaume kuna washiriki 936 huku kukiwa na washiriki 338 wa kike.
Ameongeza kuwa, mashindano hayo yatakuwa katika viwango 10 tafauti vifuatavyo; Kuhifadhi kikamilifu Quran, tafsiri na kusoma suratul A'ala, kuhifadhi juzuu 25 za Quran pamoja na Tajwid na tafsiri ya suratu al-Dhuha, kuhifadhi juzuu 20 za Quran na tajwid pamoja na tafsiri ya suratul Fil, kuhifadhi juzuu 15 na tajwid, kuhifadhi juzuu 10 za mwisho za Quran, kuhifadhi juzuu 5 za mwisho za Quran pamoja na tajwid na kuhifadhi juzuu 3 za mwisho za Quran pamoja na tajwid.
Kiwango cha nane cha mashindano hayo kimeandaliwa kwa ajili ya watu wenye zaidi ya umri wa miaka 15 ambapo washiriki watashindana katika kusoma Quran kamili. Kiwango cha tisa kitawajumuisha watu walio na umri wa kati ya miaka 9 - 14 na maqari au wasomaji watashindana katika kusoma juzuu 15 za Quran. Kiwango cha 10 kimetengwa kwa ajili ya walio na umri wa chini ya miaka 8 ambapo washiriki wanashindana katika kusoma juzuu ya 30 ya Qurani Tukufu. Mashindano hayo yataendelea hadi alhamisi ya wiki hii. 318327
captcha