IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani ya Wanachuo wa Kiislamu:

Wasomaji wa Iran, Misri na Iraq watia fora

11:42 - November 12, 2008
Habari ID: 1707414
Wawakilishi wa Iraq, Iran na Misri katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Tukufu ya Wanafunzi Waislamu wa Vyuo Vikuu wametia fora katika usomaji wa kuvutia wa Quran na kuonyesha mchuano mkubwa unaotawala mashindano hayo.
Msomaji wa kwanza katika uwanja wa qiraa alikuwa Muhammad Hamid Abdullah kutoka Bangladesh ambaye alikabiliwa na matatizo ya kiufundi katika faini hiyo. Mwanachuo huo kutoka Bangladesh pia alikuwa na makosa mengi katika kisomo cha tajwidi na usomaji sahihi wa herufi za aya za Quran.
Msomaji wa pili alikuwa Islamuddin Grayev kutoka Georgia ambaye alishiriki katika fani ya kuhifadfhi Qurani nzima. Msomaji huyo alikuwa na ufasaha mkubwa katika kusoma aya za Quran na alitumia lahani ya kisomo cha marehemu Muhammad Siddiq Minshawi. Hata hivyo alikosea kwa kusahau baadhi ya aya alizoulizwa.
Msomaji Qurani kijana kutoka Iraq Hussein al Halw aliwavutia wengi katika fani ya kusoma Qurani nzima na tangu sasa anatabiriwa kuwa mmoja wa wasomaji wenye bahati kubwa ya kupata nafasi za kwanza za mashindano hayo.
Msomaji mwingine aliyetia fora katika siku ya kwanza ya mashindano hayo ni Muhammad Hassan Muwahhidi ambaye pia anatabiriwa kuwa miongoni mwa wasomaji wenye nafasi kubwa ya kuingia fainali za mashindano hayo na kuwania nafasi ya kwanza katika fani ya tajwidi.
Mwakilishi wa Ivory Coast katika mashindano ya sasa ya kimataifa ya Quran hakufanikiwa kuwashawishi hadhirina kwa kukosea kosea katika masuala ya kiufundi. Abdullah Kamara hakufanya vizuri katika kuchagua sauti ya kuanzia kisomo chake cha Qurani Tukufu.
Msomaji Ayanuddin Hakim kutoka Uingereza pia amethibitisha kwamba mashindano ya mwaka huu ya wanafunzi wa Kiislamu wa vyuo vikuu kutoka nchi mbalimbali yatakuwa na mchuano mkubwa.
Msomaji wa mwisho kabla ya swala ya Magharibi kwa wakati wa Tehran alikuwa kutoka Misri. Muhammad Niyadhi ana sifa zote za msomaji hodari na mwenye kuzingatia masuala ya kiufundi. Alikuwa na sauti ya kuvutia mno na ni mmoja wa wasomaji wanaotarajiwa kuingia fainali za mashindano hayo. 319176

captcha