IQNA

Mashindano ya Kimataifa ya Wanafunzi Waislamu wa Vyuo Vikuu:

Kigezo changu katika kusoma Qur’ani ni sauti ya Sheisha

14:41 - November 15, 2008
Habari ID: 1708412
Msomaji Qur’ani wa Misri Junaid bin Adrus amesema kuwa sauti ya kuvutia ya sheikh Abul Einein Sheisha, Mkuu wa Jumuiya ya Wasomaji na Mahafidhi wa Qur’ani wa Misri ndiyo kigezo chake katika usomaji wa Qur’ani.
Junaid bin Adrus ambaye alikuwa akizungumza na mwandishi wa IQNA amepongeza maamuzi sahihi ya majaji wa Mashindano ya Kimataifa ya Qur’ani Wanafuzi wa Vyuo Vikuu mjini Tehran na akasema, utendaji wa kamati ya majaji wa mashindano hayo umeridhisha mno.
Msomaji huyo wa Quran kutoka Misri amesema, hii ni mara yake ya kwanza kuhudhuria mashindano ya kimataifa ya wanafunzi wa vyuo vikuu na kwamba ameshangazwa mno na jinsi viongozi na wananchi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran wanavyozingatia na kutoa umuhimu mkubwa kwa Qur’ani Tukufu.
Kuhusu kupata kwake nafasi ya tatu katika mashindano ya kusoma Qur’ani, Bin Adrus amesema, uhodari wa wasomaji mashuhuri wa Kimisri kama Ahmad Nuaina na Abul Einein Sheisha ndiyo sababu ya mafanikio ya wasomaji Qur’ani wa Kimisri na kwamba wawakilishi wa Misri wamekuwa wakipata nafasi za juu katika mashindano ya kimataifa ya Qur’ani Tukufu.
Duru ya pili ya Mashindano ya Kimataifa ya Qura’ani ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu yalimalizika jana mjini Tehran . 320050

captcha