Kikao cha siku kumi kinachofanyika chini ya anwani 'Uislamu na Amani' kwa madhumuni ya kuchunguza nafasi ya Uislamu katika kueneza amani na kuishi pamoja kwa amani katika jamii ya mwanadamu, kilianza siku ya Ijumaa tarehe 14 huko mjini Bombay India.
Moja ya malengo ya kikao hicho ni kuondoa mitazamo mibaya na isiyo sahihi ilioenea ulimwenguni kuhusiana na Uislamu. Zakir Naik, Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu ya India amesema katika siku ya kwanza ya kikao hicho kwamba, sura ambayo imekuwa ikienezwa ulimwenguni katika miaka ya hivi karibuni kuhusiana na Uislamu si sahihi, bali imepotoshwa kwa makusudi. Amesema lengo la kikao hicho si kuwabebesha watu wengine fikra za washiriki bali ni kutoa ujumbe wa Uislamu halisi kwa walimwengu. 'Uadilifu kwa ajili ya amani', 'haki za binadamu' na 'nafasi ya dini katika uutulivu wa jamii' ni miongoni mwa maudhui ambazo zitachunguzwa katika kikao hicho. 320379