IQNA

Chombo cha habari cha Kiislamu kuanzishwa barani Ulaya

12:40 - November 16, 2008
Habari ID: 1708742
Wawakilishi wa vyombo vya habari vya Kiislamu barani Ulaya wamekutana mjini Madrid, Uhispania kujadili suala la kuanzisha chombo kimoja cha habari cha Kiislamu barani humo.
Mkutano huo ambao ulitayarishwa na Mkurugenzi wa kituo cha upashaji habari cha Web Islamica cha Uhispania ulihudhuriwa na wawakilishi wa vyombo 30 vya habari vya Waislamu kutoka nchi mbalimbali za Ulaya.
Mkurugenzi wa kituo cha upashaji habari cha Safir News cha Ufaransa Muhammad Calin amesema kuwa lengo la kuanzisha chombo kimoja cha habari cha Kiislamu barani Ulaya ni kutayarisha uwanja mzuri wa kuutambulisha vema Uislamu na kupasha habari sahihi kuhusu dini hiyo.
Washiriki wa mkutano huo pia walijadili kadhia ya kubuni “hati ya thamani” zitakazotawala chombo hicho cha habari cha Kiislamu ambayo itategemea uhuru wa kujieleza.
Karibu Waislamu milioni 20 wanaishi barani Ulaya. Ufaransa ndiyo inayoongoza kwa kuwa na jamii kubwa zaidi ya Waislamu barani Ulaya kwa kuwa na Waislamu milioni tano. Inafuatiwa na nchi za Uingereza na Ujerumani ambazo kila moja ina jamii ya Waislamu milioni tatu. 320482

captcha