IQNA imenukuu Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu cha Washington kwamba msingi mkuu wa ratiba hiyo mpya ni "Qur'ani na matumizi yake katika zama za sasa."
Ratiba hiyo ya hotuba hufanyika kila Ijumaa kwa kufunguliwa na hotuba ya Sheikh Abduljalil Issa ambaye ni mmoja wa wanachama wa Kituo cha Mafunzo ya Kiislamu mjini Washington.
Kituo hicho pia kina ratiba za mafunzo ya tafsiri ya Qur’ani, elimu ya akhlaki, kisomo cha dua Kumail, masomo juu ya visa vya Qur’ani, mafunzo ya kitabu cha Nahjul Balagha na kipindi cha maswali na majibu katika siku tofauti za wiki. 321099