IQNA

Matangazo ya 'Islam Channel' nchini Afrika Kusini

11:04 - November 17, 2008
Habari ID: 1709146
Televisheni ya 'Islam Channel' itaanza kupeperusha hewani vipindi vyake nchini Afrika Kusini kuanzia mwezi Februari mwakani kwa lengo la kuwafundisha wasiokuwa Waislamu mafundisho ya dini hii tukufu.
Vipindi vya televisheni hiyo ambavyo vilianza kurushwa hewani mwaka 2004 huko nchini Uingereza, vinajumuisha matangazo ya habari, masuala ya siku na vipindi vingine vya burudani vya Kiislamu. London ndiyo makao makuu ya televisheni hiyo ambayo inarusha vipindi vyake katika nchi za Ulaya, Mashariki ya Kati na nchi za kaskazini mwa bara la Afrika. Akizungumza na gazeti la Times, Muhammad Ali, mkurugenzi wa televisheni hiyo ya satalaiti amesema kuwa, televisheni hiyo ni daraja la kuwaunganisha Waislamu na wasiokuwa Waislamu. Akiashiria idadi kubwa ya watazamaji wanaotazama vipindi vya televisheni hiyo ameongeza kuwa, kuna watu wengi tu wasiokuwa Waislamu ambao hutazama vipindi vya televisheni hiyo kutokana na kuwa ni vya kuvutia na kuchangamsha. Muhammad Ali amesema, kwa kutangaza kipindi cha 'muungano na amani duniani' kila mwaka nchini Uingereza, televisheni hiyo inafanya jitihada za kuongeza kiwango cha maarifa na ufahamu katika tamaduni nyinginezo kuhusiana na mafundisho ya Kiislamu. Muhammad Ali pia ameashiria kuongezeka kwa vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu ulimwenguni na kusema kuwa, kwa kuzingatia kuwa watu wengi ulimwenguni hawana habari sahihi kuhusiana na hali ya wanawake wa Kiislamu televiehseni hiyo imetayarisha vipindi maalumu kwa ajili ya kuondoa picha hiyo potofu na kuwasilisha picha sahihi kuhusiana na wanawake katika Uislamu. 321017
captcha