IQNA

Kuzinduliwa simu ya huduma za kiusalama kwa mahujaji mjini Makka

11:11 - November 17, 2008
Habari ID: 1709155
Said bin Abdallah al-Qahtani, mkuu wa polisi ya mji mtakatifu wa Makka ametangaza kuzinduliwa laini mahsusi ya simu nambari 987 kwa ajili ya kutoa huduma za kiusalama kwa mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu ,al- Kaaba Tukufu, katika kipindi chote cha msimu wa hija.
Al-Qahtani amesema kuhusiana na suala hilo kwamba, laini hiyo ya simu itakuwa ikifanya kazi kwa masaa 24 na kwamba iko tayari kupokea ujumbe na maombi ya mahujaji kuhusiana na masuala ya usalama wao. Amesema laini hiyo ya simu imezinduliwa kwa uungaji mkono wa Naif bin Abdul Aziz, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Saudi Arabia ambaye pia ni mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Mahujaji na kwamba lengo lake kuu ni kuharakisha mwenendo wa shughuli na hatua za kiusalama za vyombo vya usalama katika kutoa huduma kwa mahujaji. Al-Qahtani amesema mwishoni kwamba, huduma za simu hiyo zitatolewa tu katika miji mitakatifu ya Makka na Madina na hadi kufikia mwisho wa msimu huu wa hija. 321172
captcha