Mwandishi wa IQNA amesema, wasomi na wanazuoni kutoka nchi mbalimbali duniani watajadili na kubadilishana mawazo kuhusu suala la mazungumzo kati ya Uislamu na Magharibi katika kikao hicho. Gazeti la al Khalij la Umoja wa Falme za Kiarabu limeripoti kuwa Mshauri wa Masuala ya Kidini na Kisheria wa serikali ya Imarati Ali al Hashimi atawakilisha nchi hiyo katika kikao hicho.
Ali al Hashimi ameashiria ujenzi wa msikiti wa Sheikh Zayid katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Oxford na akasema, ujenzi wa msikiti huo umo katika awamu zake za mwisho. 321194