IQNA

Mahujaji wa Gaza wanasubiri viza za Saudia

10:58 - November 18, 2008
Habari ID: 1709560
Talib Abu Shi'r, Waziri wa Wakfu na Masuala ya Kidini wa Palestina imevitaka vyombo husika vya Saudi Arabia kutoa viza za kuzuru Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwa mahujaji wa Kipalestina wanaokaa katika Ukanda wa Gaza.
Amesema katika hali ya hivi sasa Wapalestina wanaoishi katika Ukanda huo wanasubiri kwa hamu kubwa viongozi wa Saudi Arabia wachukue hatua za haraka ili kuharakisha utoaji viza kwao ili waweze kutekeleza ibada yao ya hija kwa wakati. Waziri huyo wa Palestina amesema kuwa wizara yake ilichukua hatua za lazima mapema ili kuwawezesha Wapalestina kuhiji kwa wakati. Amesema karibu Wapalestina 19,200 wakazi wa Gaza wamejiandikisha kufanya safari katika ardhi takatifu ya Makka katika msimu huu wa hija ambapo watu 3200 wamechaguliwa kupitia kura kushiriki katika ibada hiyo muhimu ya Mwenyezi Mungu. Wakati huohuo, Awadh Abu Madhkur, mkuu wa shughuli za hija wa Palestina amewataka viongozi wa Saudi Arabia kuchukua hatua za haraka ili kutoa viza kwa wakati kwa Wapaletina wa Gaza walioazimia kutekeleza hija mwaka huu. Pia amewataka viongozi wa Misri kufungua kivukio cha Rafah ili kurahisisha shughuli za Wapalestina wanaotaka kwenda Makka kwa ajili ya kufanya hija. 321509
captcha