Waziri Saleh bin Abdulaziz Al Sheikh amesema, mpango huo unatekelezwa kwa ushirikiano wa vyombo vya habari na taasisi za ulinganiaji za Saudi Arabia.
Amesema kuwa sehemu moja ya mpango huo inahusu ugawaji wa vitabu vinavyofafanua ibada ya hija kwa zaidi ya lugha 25 za kigeni, hotuba, makongamano na mikutano ya kuwaelimisha mahujaji njia sahihi za kutekeleza amali za hija.
Waziri wa Waqfu wa Saudia amesema kuwa walinganiaji waliowekwa kwenye ofisi za Wizara ya Waqfu ya Saudi Arabia katika miji ya Makka na Madina na vituo mbalimbali vilivyotayarishwa kwa ajili ya shughuli hiyo, watakuwa wakijibu maswali ya kisheria ya mahujaji kuhusu kanuni na wajibu za hija na vitendo vilivyokatazwa kufanya wakati wa ibada hiyo.
Al Sheikh amesema kuwa, mpango huo unatekelezwa kwa mwaka wa pili sasa katika msimu wa ibada ya hija. 321638