Baraza hilo limesema kuwa kati ya askari wote 2347 wanaohudumu katika sekta ya mapambano dhidi ya ugaidi ya nchini Uingereza, ni askari 27 tu wa Kiislamu ndio wanaohudumu katika sekta hiyo, na kwamba kati ya polisi wakaguzi 4630 ni 30 tu kati yao ndio Waislamu jambo linaloonyesha kwamba idadi ya Waislamu katika kikosi kizima cha polisi ya Uingereza ni ndogo mno. Kwa mujibu wa baraza hilo la polisi wa Kiislamu, polisi ya Uingereza inapasa kuongeza idadi ya askari Waislamu nchini humo ili kuwashirikisha Waislamu katika juhudi za kupambana na magaidi na watu wenye misimamo ya kupindukia mipaka.
Tunakumbusha hapa kwamba katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, Tariq Ghafur mmoja wa polisi wa Kiislamu wa Uingereza alishukuriwa na polisi ya Uingereza kutokana na hatua yake ya kulalamika na kuwashtaki mahakamani wakuu wake waliokuwa wakimfanyia vitendo vya ubaguzi wa rangi. Alikuwa akitaraji kuwa angepewa nafasi ya kusimamia kikosi cha askari usalama watakaosimamia michezo ya olimpiki iliyopangwa kufanyika nchini humo mwaka 2012, lakini amestaafu kabla ya kufanyika michezo hiyo. 321564