Maimamu hao wamehitimu masomo yao katika taasisi hiyo ya al-Ghazali baada ya kujishughulisha na masomo kwa kipindi cha miaka minne na kutumia muda mwingine katika kupata elimu katika chuo cha Kanisa Katoliki cha mjini Paris. Sherehe za maimau hao kupata vyeti vyao zitafanyika katika Msikiti wa Paris. Wanawake watatu ni miongoni mwamaimamu hao watakaopewa vyeti vya kuhitimu masomo. Katika mahojiano yake na gazeti ka Le Mond, Muhammad Musawi, Mkuu wa Baraza la Waislamu wa Ufaransa ameashiria uhaba wa vyuo vya kutoa mafunzo kwa maimamu wa swala ya jamaa nchini humo na kuongeza kuwa, baraza hilo limeazimia kuwatuma nchini Morocco vijana wa Kiislamu walio na hamu ya kujifunza masomo ya Kiislamu. Kuhusiana na suala hilo, katika mwezi wa Ramadhani uliopita, maimamu zaidi ya 150 wa swala ya jamaa walitumwa nchini Ufaransa kutoka Morocco kwa ajili ya kuswalisha swala hiyo na vilevile kuhubiri Uislamu. Kwa mujibu wa Wizaraya Mambo ya Ndani ya Ufaransa, nchi hiyo ina misikiti na sehemu za kuswalia zipatazo 2890, na kwamba kwa kuwa na zaidi ya wafuasi milioni tano, Uislamu ndiyo dini ya pili kwa ukubwa nchini humo baada ya Kanisa Katoliki. 323410