Akizungumza na gazeti la nchi hiyo la ar-Rayah, Abdallah an-Najjar, Mkurugenzi Mwandamizi wa Jumuiya ya Majumba ya Makumbusho ya Qatar amesema kuwa karibu shakhsia wa siasa na sanaa wapatao 1000 wamealikwa kuhudhuria sherehe za ufunguzi wa jumba hilo. Ameongeza kuwa Amir Sheikh Hamad bin Khalifa Aal Thaani wa Qatar, Ekmeleddin Ihsanoglu, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiislamu OIC, Amr Musa, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Rais Bashar Asad wa Syria ma mabaolzi wa nchi zote za kigeni wanaohudumu nchini Qatar ni miongoni mwa shakhsia walioalikwa kushiriki katika sherehe hizo. An-Najjar amesema kuwa karibi athari 1000 za Kiislamu zilizokusanywa katika kipindi cha miaka 1300 zimehifadhiwa katika jambo hilo, jambo linaloonyesha utajiri mkubwa wa sanaa na uvumbuzi wa Kiislamu. Akisisitiza kuwa jumba hilo la makumbusho ni hatua muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu, An-Najjar ameongeza kuwa athari na vitu vya kihistoria vilivyokusanywa katika jumba hilo vimekusanywa kutoka katika nchi mbalimbali zikiwemo za Misri, Iran, Syria, Iraq, Uturuki, India, Hispania na nchi nyingine nyingizo za dunia. Amesema kuwa mbali na athari za kale, kuna vitabu na nuskha zilizoandikwa kwa miandiko mbalimbali ya kale ambazo zimekusanywa na kuhifadhiwa kwa ustadi mkubwa katika jumba hilo. Wataalamu wa mambo ya kale walioshiriki katika sherehe za ufunguzi wa jumba hilo wamesema kuwa kufunguliwa kwa jumba hilo nchini Qatar kunaonyesha wazi jinsi nchi hiyo inavyojali kulindwa urithi wa ustaarabu, utamaduni na historia ya Kiislamu. 323720