Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan amelaani mwenendo unaoendelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel wa kuchimba mashimo, kubomoa na kujenga mifereji chini na kandokando ya msikiti wa al Aqsa na Quds Tukufu huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Mwandishi wa IQNA huko Jordan amesema kuwa Waziri Salahuddin al Bashir amelaani uhalifu huo na kusema, vitendo hivyo vya Israel vinakiuka maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Baraza Kuu la umoja huo na sheria zote za kimataifa hususan makubalino ya mwaka 1949 ya Geneva.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jordan amesema kuwa hatua hizo za utawala ghasibu wa Israel zitabadilisha utambulisho wa eneo la mashariki mwa Quds na akaongeza kuwa vitendo hivyo vitakuwa na taathita hasi katika mwenendo wa kutafuta suluhisho la kudumu la suala la Quds na kufikiwa amani ya kweli Mashariki ya Kati.
Salahuddin al Bashir ametaka kusimamishwa uchumbaji wa mashimo chini ya msikiti wa al Aqsa. 322712