Kwa mujibu wa gazeti la as-Sharq wawakilishi wa nchi za Kuwait, Saudi Arabia, Qatar, Imarati, Bahrain na Oman wanashiriki katika mashindano hayo yanayoendelea katika mji wa Doha. Washiriki wa kiume na wa kike wanashiriki katika makundi tofauti ya kuhifadhi Qur’ani na hadithi katika mashindano hayo. Jana vijana wenye umri wa kati ya miaka 15 hadi 25 walishiriki katika mashindano hayo kwa kusoma sura za Maryam, Taha, Anbiyaa, Haj na Mu’minun. Vijana wenye umri uliotajwa, kesho watashindana kuhifadhi sura za Yunus na Hud ilhali wale wenye umri wa miaka 10 hadi 14 watasoma sura za Ankabut na Rum kwa mtindo wa tajweed. Maonyesho ya vitabu, majarida na magazeti ya Kiislamu pia yanaonyeshwa pembeni mwa mashindano hayo. Mashindano hayo ya 21 yaliyoandaliwa na Idara Kuu ya Masuala ya Vijana ya Wizara ya Utamaduni ya Qatar, yanatazamiwa kufungwa rasmi siku ya Jumanne. 324323