Kwa mujibu wa Mtandao wa Intaneti wa Darul Seyyedat Ruqiya Al Quran Al Karim, katika makala yake, Sheikh Abdullah ameashiria namna Warumi waliovyoangamizwa na Wairani kwa mujibu wa aya za pili na tatu za Surat-Ar-Rum katika Qur'ani Tukufu zisemazo: " Warumi wameshindwa. Katika nchi iliyo karibu. Nao baada ya kushindwa kwao watashinda". Anasema utabiri wa Qur'ani ulikuwa wa kweli kabisa na kuongeza kuwa: " Kisimamo cha dunia cha Qaim Al Muhammad SAW ni utabiri ulio kweli katika Qur'ani na kuongeza kuwa kuna zaidi ya aya 106katika Quran tukufu ambazo wafasiri wa Qur'ani wanasema, Maimamu Maasumu AS wameashiria kwamba zinathibitisha kudhihiri Imam Mahdi (ATF) katika zama za mwisho.
Katika sehemu nyingine ya makala yake anachunguza aya za tano na sita za Sura Qasas zisemazo: " Na tukataka kuwafadhili waliodhoofishwa katika nchi (ardhi) hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi. Na kuwapa nguvu katika nchi, na kutokana na wao kuwaonyesha kina Firauni na Hamana na majeshi yao mambo yale waliyo kuwa wakiyaogopa." Sheikh Abdullah anachambua aya hizo na kunukulu kitabu cha Al Ghaiba cha Sheikh Tousi anayetegemea riwaya za Maimamu Watukufu AS na kuandika: "Waliodhoofishwa katika nchi (ardhi)" ni watu wa Nyumba ya Mtume Muhammad SAW ambao Mwenyezi Mungu kupitia kisimamo cha dunia cha Imam Mahdi ATF atawaongezea ezi na kuwadhalilisha maadui zao.
Mwanazuoni huyo wa Syria ananukulu kitabu cha Maani al Akhbar cha Sheikh Swaduq anayetegemea riwaya ya Imam Sadeq AS na kuandika: "Mtume SAW aliulizwa kuhusiana na aya hizo za tano na sita za Suratul Qasas, na huku akitokwa na machozi aliwaashiria Ali AS, Hassan AS na Hussein AS na kusema, watakuwa Maimamu baada yake na kuwataja kuwa " waliodhoofishwa katika ardhi."
Sheikh Abdullah katika kuendelea na makala yake anasema, neno "Firauni" linatumika kama nembo ya kuarifisha watawala madhalimu ambao huibuka katika kila zama na katika kila umma. Na kuhusu "kina Firauni na Hamana na majeshi yao" anawanukulu Imam Baqir AS na Imam Swadiq AS na kuandika: "Aya hizi zinaashiria watu wawili madhalimu ambao pamoja na wafuasi wao watafufuliwa na Mwenyezi Mungu katika zama za mwisho ambapo kupitia kisimamo cha Imam Mahdi (ATF) atalipiza kisasi kutokana na udhalimu waliofanya huko nyuma.
Mwanazuoni huyo mwishoni mwa sehemu ya kwanza ya makala yake ananukulu aya ya 55 ya Suratun Nur isemayo: "Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia dini yao aliyowapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watakao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu." Anasema, aya hii kuwa ambayo inatoa dalili za kisimamo cha dunia cha Imam Mahdi ATF.
Sheikh Abdullah anamaliza makala yake kwa kunukulu kitabu cha Ghayat Al Maram cha Sheikh Bahrani ambaye anategemea riwaya za Imam Ali AS na kuandika: "Ahadi aliyotoa Mwenyezi Mungu katika aya hii inakaribia na siku hiyo itafika ambapo Uislamu hautabakia isipokuwa jina na Qur'ani, na hakitabakia chochote katika kitabu cha Qur'ani isipokuwa mandishi yake. Ni katika zama hizo ndio Imam wa Zama atadhihiri kutoka ghaiba kutokana na kuvunjwa ahadi na kuenea fitina. Watu watakaonekana kuwa karibu naye watageuka na kuwa maadui na katika zama hizo Mwenyezi Mungu atamsaidia na kupitia kiamu chake ataiweka wazi dini ya Mtume Wake na wote wataifahamu vyema dini.
Msomi huyu wa Kishia alimaliza muhadhara wake kwa kunukulu riwaya ya Imam Sadiq AS katika kitabu cha Maani Al Akhbar cha Sheikh Swaduq kuhusu aya ya 55 ya Suratun Nur na kuandika: "Hii aya inamhusu Imam Ali AS na Maimamu Watukufu AS ambao ni watoto wake na inahusu pia kudhihiri Imam Mahdi ATF.
Inaendelea
323271