IQNA

Kikao cha kwanza cha mamufti wa ulimwengu wa Kiislamu mjini Makka

8:18 - December 01, 2008
Habari ID: 1714344
Abdullah bin Abdul Muhsin at-Turki, Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kimataifa ya Uislamu amezungumzia mipango ya kufanyika kikao cha kwanza cha mamufti wa ulimwengu wa Kiislamu hivi karibuni mjini Makka Saudi Arabia.
Gazeti la nchi hiyo la al-Watan limemnukuu at-Turki akisema jana kwamba, kikao hicho kitasimamiwa na Mfalme Abdallah bin Abdul Aziz wa nchi hiyo. Amesema kuwa mbali na mamufti wa nchi za Kiislamu, mamufti wa jamii za Kiislamu wa nchi zisizokuwa za Kiislamu pia watashiriki katika kikao hicho. Amesema kuwa hitilafu za fatuwa zinazotolewa na manazuoni wa Kiislamu zimemesababisha baadhi ya matatizo katika jamii za Kiislamu na wakati huohuo hitilafu hizo kutumiwa vibaya na maadui wa Uislamu dhidi ya Waislamu. At-Turki amesema, si mamufti wote wanaotoa fatuwa katika ulimwengu wa Kiislamu wanafaa kufanya hivyo na kusisitiza kwamba, katika kikao hicho cha Makka, mipango itafanyika ili kuratibu njia za utoaji fatuwa katika masuala tofauti ya kisheria na kuzuia utolewa wa fatuwa zisizofaa katika kanali za televisheni za satalaiti. At-turki amesema, mazungumzo ndiyo njia bora zaidi ya jamii za Waislamu kufahamiana na kuelewa vyema misingi ya mafundisho ya dini yao tukufu, na kuwataka wanazuoni, wasomi na watafiti wote wa Kiislamu kufanya juhudi zaidi za kutafuta njia za kuimarisha mazungumzo kati ya dini na tamaduni mbalimbali. 327735
captcha