IQNA

Waidhi asisitiza kuimarishwa shughuli za Qur'ani kati ya Iran na Sudan

8:17 - December 01, 2008
Habari ID: 1714348
Muhammad Waidhi, Naibu Mkuu wa Taasisi ya Utamaduni na Mawasiliano ya Kiislamu ametaka kuimarishwa shughuli za Qur'ani kati ya Iran na Sudan, baada ya kuitembelea Jumuiya ya Qur'ani Tukufu ya nchi hiyo.
Ibrahim Anzwar, Mkuu wa Kitengo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Sudan amesema kuwa, Waidhi pia amekutana na mkuu wa Chuo Kikuu cha Qur'ani na Hadithi cha Sudan na baada ya kuarifishwa shughuli za chuo hicho akatangaza kuwa tayari tasisi za Qur'ani za Iran kushirikiana na chuo kikuu hicho katika shughuli mbalimbali za Qur'ani Tukufu ikiwa ni pamoja na kutumwa jumbe mbalimbali za Qur'ani ili kushiriki katika mashindano tofauti ya kimataifa. Mkuu wa chuo hicho alitoa ripoti fupi kuhusiana na hatua tofauti zinazopitiwa na vijana wa Sudan katika kusoma na kuhifadhi kitabu hicho kitakatifu.327459
captcha