IQNA

Sheikh wa al-Azhar: Sikumjua Peres nilipokuwa nikimpa mkono

10:24 - December 03, 2008
Habari ID: 1715366
Ofisi ya Muhammad Sayyid Tantawi, Sheikh Mkuu wa al-Azhar, imetoa taarifa ikidai kwamba sheikh huyo hakumjua Shimon Peres Rais wa utawala haramu wa Israel alipokuwa akimpa mkono wakati wa kumsalimia huko New York, pambizoni mwa kikao cha kimataifa cha mazungumzo ya kidini.
Taarifa hiyo imesema kuwa, baadhi ya habari zinazoenezwa na vyombo vya habari kuhusiana na jambo hilo si za kweli na kwamba kukutana kwa viongozi hao wawili kulikuwa ni kwa ghafla kabisa bila ya kuwepo mipango yoyote ya awali. Taarifa hiyo imeendelea kudai kwamba, baada ya Ban Kii Moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuwashukuru washiriki wa mkutano huo, shakhsia na viongozi wengi, akiwemo Peres, walimwendea Sheikh Tantawi ili kumsalimu, na kwamba kusalimiana viongozi wawili hao kulitimia ghafla na bila ya Sheikh Tantawi kumfahamu kiongozi huyo katili wa Israel ambaye anaendelea kuwachinja kinyama na bila huruma Wapalestina. Sheikh al-Azhar pia ametoa madai kama hayo katika mahojiano yake na gazeti la Kuwait la al-Jazeera. Kitendo cha sheikh huyo kumpa mkono Peres kimekabiliwa na radiamali kali ya vyombo vya habari na wabunge wa Misri, taasisi za Kiislamu na shakhsia wengi katika ulimwengu wa Kiislamu ambao wamesema kuwa ni cha dharau na matusi kwa Waislamu na hasa wananchi madhlumu wa Palestina. Wabunge na shkhsia kadhaa wa kisiasa wa Misri wametoa taarifa tofauti wakitaka kuuzuliwa kwa Tantawi kutoka kwenye nafasi yake hiyo ya kuwa Sheikh wa al-Azhar. Iwapo tutafaradhisha kuwa madai hayo ya Tanyawi ni sahihi, basi kuna haja kubwa kwa viongozi wa taasisi hiyo muhimu katika ulimwengu wa Kiislamu kunyanyua kiwango chao cha kisiasa ili kupata kutambua sura ya makatili wakubwa kama vile Shimon Peres, ambaye anatambuliwa mara moja na hata mtu yoyote yule asiyekuwa na muamko wala ujuzi wa habari zinazotekea kila siku ulimwenguni.328770
captcha