IQNA

Warsha ya mafunzo kwa wanazuoni wa Pakistan

10:21 - December 03, 2008
Habari ID: 1715371
Warsha ya mafunzo kwa ajili ya wanazuoni wa Kiislamu wa Pakistan ilianza Jumatatu huko katika mji wa Lahore. Warsha hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Sheikh Zahid ya Chuo Kikuu cha Punjab cha nchini Pakistan.
Kwa mujibu wa tovuti ya The News, Mujahid Komran, Mkuu wa zamani wa Chuo kikuu hicho ameishukuru Taasisi ya Sheikh Zahid kwa kuandaa warsha hiyo, na kusema kuwa warsha hiyo inaweza kuwa na nafasi muhimu katika kuwaelimisha na kuwakumbusha wanazuoni majukumu yao mazito katika kukabiliana na propaganda sumu zinazoenezwa ulimwenguni na maadui wa Uislamu.
Amesema, hii leo kuna propaganda nyingi potofu zinazoenezwa kwa makusudi dhidi ya Uislamu na maadui na hasa nchi za Magharibi na kusisitiza kwamba, kwa kuzingatia suala hilo kuna udharura mkubwa kwa wanazuoni kupanga mikakati na mbinu za kukabiliana na hujuma hiyo isiyo ya kiuadilifu. 328866
captcha