IQNA

Kujitenga na Qur'ani ndiyo sababu kuu ya hitilafu kati ya Waislamu

10:36 - December 03, 2008
Habari ID: 1715378
Waislamu katika maeneo mbalimbali ya dunia hawaishi katika amani na utulivu na hitilafu zimeenea kati ya wafuasi wa makundi na madhehebu mbalimbali za Kiislamu suala ambalo linatokana na kujitenga kwao na Qur'ani Tukufu na mafundisho ya kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.
Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Fiqhi ya Kiislamu ya India Khalid Saifullah katika kongamano la kuuarifisha Uislamu katika nchi zisizokuwa za Kiislamu unaofanyika mjini Makka. Sheikh Khalid Saifullah amesema, kutekeleza sheria za Qur'ani na kuwalingania watu mafundisho ya mwenyezi Mungu ni faradhi ambayo Waislamu wote wanawajibika kuitekeleza.
Katibu Mkuu wa Kamati ya Kuuarifisha Uislamu ya Kuwait ambaye pia amewasilisha makala katika kongamano hilo Muhammad Ismail al Ansari amehimiza juu ya umuhimu wa kulingania dini ya Kiislamu kwa wasiokuwa Waislamu. Hata hivyo amesema, katika kipindi cha sasa si jambo rahisi kulingania Uislamu katika nchi za Magharibi kwani fikra za waliowengi katika nchi zisizokuwa za Kiislamu hususan baada ya mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001 huko Marekani zimetwishwa picha mbaya dhidi ya Uislamu na Waislamu. Amesisitiza kuwa vyombo vya habari vya Magharibi pia vinafanya propaganda kubwa za kuchafua sura halisi ya Uislamu.
Muhammad Ismail al Ansari amezitaka jumuiya za Kiislamu kutangaza Uislamu kwa wasiokuwa Waislamu na kufafanua misingi ya dini hiyo na thamani zake kupitia njia ya kuanzisha televisheni za satalaiti na kuchapisha magazeti na majarida kwa lugha mbalimbali. 328804
captcha